Back to top

Auawa na mume wake baada ya kudai fedha za ada ya mtoto, Iramba.

22 July 2021
Share

Mwanamke mmoja Mkazi wa Kijiji cha Ndulungu Wilayani Iramba ameuwawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake, baada ya kudai fedha za ada ya mtoto wake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Bi.Stella Mutabihirwa amesema tukio hilo limetokea baada ya Bibi Moshi Rashidi mwenye umri wa miaka arobaini kuomba fedha walizouza mahindi na kukubaliana na mume wake zitumike kwa ada ndipo akaangushiwa kipigo.