Back to top

Aweso awasimamisha kazi meneja wa maji RUWASA mkoa wa Mara na Tarime.

06 January 2021
Share

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewasimamisha kazi Meneja wa Wakala wa Huduma za Maji, Mjini na Vijijini mkoa wa Mara (RUWASA) Bw.Sadick Chaka pamoja na Meneja wa RUWASA wilaya ya Tarime, Marwa Muraza kwa kushindwa kusimamia miradi ya maji licha ya kuwa wana fedha zaidi ya shilingi bilioni tatu kwenye akaunti na kutoa taarifa za uongo mbele ya Waziri.