Back to top

Baba aua mwanaye kwa kumcharaza fimbo mkoani Mwanza.

26 November 2020
Share

Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamsaka Adam Athuman mkazi wa eneo la Nyamadoke wilayani Ilemela kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo mtoto wake Athuman Adam mwenye umri wa miaka 10  mwanafunzi wa shule msingi Nyamadoke.

Kamanda polisi mkoa wa Mwanza Muliro Jumanne Muliro anathibitisha kutokea kwa tukio hilo   na kusema kuwa jeshia hilo linamtafuta mhusika ili aje kujibu tuhuma zake.

Tukio hilo linatokea wakati maadhimisho ya siku 16 ya za kupinga ukatili yakiendelea duniani kote ambapo viongozi wa serikali ya mtaa alipokuwa akiishia  marehemu huyo wamekemea  ukatili huo na kuziomba mamlaka husika kuchukua hatua.

Majirani hao wamesema  mara nyingi inaaminika kuwa mikononi mwa wazazi ni sehemu salama kwa watoto, lakini tukio hili linalodaiwa kufanywa na baba mzazi wa mtoto linamewasikitisha na kuwafanya wafikirie tofauti.