Watu wawili wa familia moja baba na mtoto wake wakazi wa kijiji cha Kenyamusabi mkoa wa Mara wamejeruhiwa kwa kwa kuchomwa na mkuki na kukatwa katwa na mapanga kutokana na migogoro ya ardhi kati yao na familia ya Rhobi Daniel ambayo imetokomea kusikojulikana baada ya tukio hilo.
Akielezea tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji hicho Mwita Raphael ametaja majeruhi hao kuwa ni John Joel baba mzazi na mwingine ni Hula John mtoto wa Joel ambaye yeye amechomwa mkuki ubavuni huku baba akijeruhiwa kwa kukatwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake .