Back to top

Bajeti ya Trilioni 36.33 yakaza na kulegeza.

10 June 2021
Share

Serikali imewasilisha bajeti yake ya shilingi Trilioni 36.33 huku bajeti hiyo ikikaza na kulegeza katika maeneo mbalimbali ambapo  kodi katika mafuta ya Petroli na Dizeli imeongezeka, gharama za matumizi ya simu za mkononi zikiongezeka wakati faini ya makosa ya  boda boda ikipungua kutoka shilingi 30,000 hadi 10,000 kwa kosa moja.

Akiwasilisha bajeti hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Mwigulu Nchemba amesema bajeti hiyo imelenga kuboresha huduma mbalimbali za  kijamii na hata sehemu ambazo kodi zimeongezwa nzinalenga kwenda kuboresha huduma hizo.

Kuhusu faini za Boda boda amesema, vijana wengi wamejiajiri kwenye sekta ndogo ya kuendesha bajaji na pikipiki zikijulikana kama  bodaboda, lakini amesema vija hao hupata usumbufu mkubwa wa kulipa faini.

Aidha  Mhe.Nchemba amesema serikali inakusudia Kupunguza Ushuru wa Forodha hadi asilimia 0 kutoka viwango vya awali vya asilimia 10 na asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa vifaa maalum vinavyotumika katika kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu.