Back to top

Balozi Chipeta awasilisha hati ya utambulisho.

20 October 2022
Share

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  katika Falme ya Uholanzi , Mhe. Caroline Kitana Chipeta, awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi.


 
Hafla hiyo imefanyika katika moja ya Kasri za Kifalme iliyoko Noordeinde, The Hague,  Uholanzi .

Julai 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alimteua Balozi Caroline Kitana Chipeta kuwa Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi.