Back to top

Bangladesh kushirikiana na UNHCR kujadili suala la wakimbizi.

20 August 2019
Share

Serikali ya Bangladesh imeahidi kushirikiana na Shirika la Wakimbizi na Umoja wa Mataifa, UNHCR,kutathmini iwapo zaidi ya wakimbizi 3,000 wa jamii ya Rohingya watakubali pendekezo la Myanmar kurejea nyumbani, takribani mwaka mmoja baada ya mpango mkubwa wa kuwarejesha nyumbani kushindwa.

Serikali ya Myanmar imewaidhinisha watu 3,450 kutoka orodha ya watu 22,000 iliyotolewa na serikali ya Bangladesh, kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Myanmar, Zaw Htay.