Back to top

Barua ya wazi kwa rais Dkt.Magufuli yawafutia mashtaka ya mauaji

14 March 2019
Share

Mkurugenzi wa mashtaka nchini Biswalo Mganga amefuta kesi namba 8/2018 ya mauaji ya Jackson Thomas iliyokuwa ikiendelea kwenye mahakama ya Tabora baada ya kubaini watuhumiwa Mussa Adam Sadick na Edward Matiku Nduli walibambikiwa mashtaka hayo kinyume cha sheria

Hatua hiyo inafikiwa baada ya mmoja wa watuhumiwa Mussa Adam Sadick kuandika barua ya wazi na kuomba msaada kwa rais John Pombe Magufuli kwenye moja ya chombo cha habari kwa madai ya kukamatwa na polisi bila kosa na kufikishwa mahakamani mnamo tarehe 6/5/2018 na kusomewa shtaka la mauaji na kisha kuunganishwa na Edward Nduli ambaye alikuwa hamjui katika shtaka hilo

Barua hiyo ilisomwa na rais Magufuli ambaye aliagiza ofisi ya DPP kufuatilia kesi hiyo na ndipo ilipobaini malalamiko hayo ni ya kweli na mnamo tarehe 8/3/2019 iliwafutia washtakiwa wote mashtaka na mahakama imewaachia huru.

Aidha DPP Mganga amesema kufuatia tukio hilo rais John Pombe Magufuli ameagiza hatu kali za kisheria zichukuliwe kwa waliohusika ili kukomesha tabia hizo zinazoichafua serikali kwa wananchi wake na dunia nzima