Back to top

Bashe achukizwa na utaratibu unaotumika kuwakopesha wakulima.

05 August 2020
Share


Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe amesema wizara hiyo inaandaa sera ya fedha ya kuwakopesha wakulima itakayokuwa rafiki kwa wakulima.

Kwa sera au utaratibu wa sasa, mkulima anakopeshwa kwa kutakiwa kuurejesha kwa kulipa riba ya asilimia kumi na nane kuanzia mwezi wa pili baada ya kuchukua, hata kama zao analotarajia kuliuza litavunwa baada ya miaka mitatu.

Mhe.Bashe amesema hayo wakati akifungua maonesho ya kilimo na Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika katika viwanja vya Nyamongolo jijini Mwanza.

Akitembelea mabanda mbalimbali, Mhe.Bashe ameonyesha kutoridhishwa utaratibu unaotumika na taasisi za fedha kuwakopesha wakulima.

Mhe.Bashe amewataka wakuu wa mikoa ya kanda ya Ziwa Magharibi waanze kutenga maeneo yatakayotolewa bure kwa vijana kwa ajili ya kilimo, ili serikali ipeleke wataalam wake katika maeneo hayo.