Back to top

Basi la Tahmeed lagongana na Lori eneo la Jogoo Dar es Salaam.

19 May 2019
Share

Abiria waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Tahmeed lenye Namba za usajili KCN 970R wamenusurika kifo baada ya basi hilo kugongana na Lori la mizigo lenye namba za usajili T235 AXJ katika eneo la Jogoo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa Mujibu wa Mashuhuda wa ajali hiyo waliozungumz na ITV Online wamesema chanzo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo lililokuwa likitoka katika kituo cha mabasi ubungo kuelekea Jijini Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Kamanda wa kikosi cha usalama bara barani wilaya ya kinondoni ASP Sadick Msangi amesema hakuna majerui aliyepata madhara katika ajari hiyo ambapo hakusema sababu za ajali hiyo kuwa ni mwendokasi huku akisema wanachunguza, ambapo ametumia nafasi hiyo kuendelea kuwaasa madereva kuwa na tahadhari pindi watumiapo vyombo vya moto barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.