Back to top

Basi lagonga lori kwa nyuma na kutumbukia korongoni Singida.

05 July 2020
Share

Zaidi ya abiria arobaini waliokuwa wakisafiri kutoka Dar-es-salaam kuelekea Kahama wamenusurika kifo huku wengine wakipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida ,baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuligonga lori kisha kutumbukia korongoni.
 
Ajali hiyo ambayo imetokea majira ya saa kumina moja asubuhi eneo la Mangua Njuki Manispaa ya Singida ,lililohusisha basi la abiria  lenye usajili wa namba T 721 DEN  na lori aina ya fuso lenye usajili wa namba T. 981 DER yote yalikuwa yakielekea Kahama , ajali hiyo imedaiwa  kusababishwa na mwendo kasi wa dereva wa basi .

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida na Daktari bingwa wa upasuaji wa mifupa daktari Deogratius Banuba amethibitisha kupokea majeruhi na kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.