Back to top

BAWACHA watishia kuandamana uwepo wa wabunge 19 wa viti maalumu Bungen

09 May 2021
Share

Baraza la Wanawake wa CHADEMA(BAWACHA) mkoa wa Ruvuma limepinga kuendelea kuwepo bungeni kwa wabunge 19 wa viti maalumu wa CHADEMA na kumtaka Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai kuwaondoa wabunge hao vinginevyo wataandamana kwenda bungeni kushinikiza kuondolewa bungeni kwa wabunge hao.
.
Katibu wa BAWACHA wa mkoa wa Ruvuma Bi. Rebeka Milinga amesema uwepo wa wabunge hao bungeni haukufuata taratibu za chama chao na hivyo wamepoteza sifa ya kuwa wabunge na kwamba hawastahili kuwepo bungeni.
.
Wanawake hao wamesema wanashangaa kuona wabunge hao bado wapo bungeni hadi leo ili hali CHADEMA iliwavua uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge.