Back to top

Benki kuu ya Tanzania yahamishia madeni ya Benki M, Banki ya Azania.

15 January 2019
Share

Benki Kuu ya Tanzania imehamisha mali na madeni yote ya benki M  kwenda benki ya Azania Limited baada ya benki hiyo kushindwa kujiendesha.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt.Benard Kibese amesema  benki M ilipewa zaidi ya miezi sita  ijiendeshe kwa mujibu wa taratibu   lakini ilishindwa kufanya hivyo.

Amesema kinachoendelea kwa sasa ni kukamilishwa kisheria ili uhamisho huo uweze kukamilika kama unavyopaswa.