Back to top

Benki ya umoja wa Ulaya yaleta neema kwa wakazi wa Mwanza

25 May 2020
Share

Wakazi wa manispaa ya Ilemela mkoani M wanza wameanza kunufaika na mradi mkubwa wa maji safi na salama uliotekelezwa na serikali kwa gharama ya shilingi billioni 119.

Baadhi ya wakazi hao wakiwemo wa kata za Kirumba, Kitangiri, Nyasaka na Nyamhongolo wameishukuru serikali kwa kuwaondolea kero ya upatikanaji wa maji safi iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu.

Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela John Wanga amesema kuimarika kwa huduma ya maji safi katika manispaa hiyo ni mpango wa serikali ya awamu ya tano wa kumtua mama ndoo kichwani katika kuondoa changamoto za sekta ya maji.