Back to top

Biashara ya Kahawa ya magendo yashamiri Mbinga.

22 September 2018
Share

Vitendo vya biashara ya magendo ya Kahawa  vimeshamiri  wilayani Mbinga mkoani Ruvuma ambapo  serikali wilayani  humo imekamata  shehena ya  Kahawa ya magendo ikiwa katika mifuko 600 ya sandarusi katika ghala bubu linadaiwa kumilikiwa na Bw. Joackim Kohelo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Bw. Juma Mnwele  amesema Kahawa hiyo  imekamatwa baada ya msako  kuwabaini watu wanaonunua Kahawa  kwa watui binafsi badala ya  kupitia kwenye vyama vya ushirika.

Kwa upande wake mtuhumiwa Joackim Kohelo amesema kuwa hakununua kahawa hiyo bali amelima kwa kushirikiana na ndugu zake.