Back to top

Biashara ya Mirungi yashamiri kwa wanafunzi wa Sekondari Longido.

18 October 2019
Share

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari ya Namanga wilayani Longido mpakani mwa Tanzania na Kenya wafanyabiashara ya haramu ya mirungi kwa madai ya uhaba wa mabweni unaowalazimu wengi wao kuishi nje ya shule.

Mkuu wa shule hiyo Mtesigwa Misana amesema mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega aliyetembelea shule hiyo kuwa  yapo mabweni matatu kati ya saba yanayohitajika, hali ambayo pia imechangia ongezeko la wanafunzi wa kike kupata ujauzito.

Wanafunzi wa shule hiyo waliozungumza na ITV wamekiri kuwa ukosefu wa mabweni umechangia kurudisha nyuma maendeleo yao wakiomba serikali na wadau wengine.

Akizungumza na wazazi wa eneo ilipo shule hiyo Mhe.Ulega amewahamasisha kuchangia kwa kasi ili kuwapa watoto wao haki ya msingi ya  elimu.