Back to top

Bilioni 25.3 zatumika kuboresha barabara za mitaa Manispaa ya Musoma.

22 September 2020
Share

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi Mhe.Kassim Majaliwa amesema shilingi bilioni ishirini na tano nukta tatu zimetumika kuboresha barabara na mitaa ya Manispaa ya Musoma ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho ya mwaka 2015/2020.

Amesema hayo alipozungumza na wakazi wa mji wa Musoma katika mkutano wa kampeni wa chama hicho mjini Musoma kuomba kura kwa ajili ya mgombea wa CCM, Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na wabunge na madiwani wa chama hicho.

Amesema shilingi bilioni kumi na nane nukta saba zimetumika kujenga kilomiya kumi na nne za barabara kwa kiwango cha lami na kuweka taa za barabarani kupitia Programu ya Uboreshaji wa Miji katika Manispaa ya Musoma na mradi umekamilika.

Mhe.Majaliwa amesema kupitia Mfuko wa Matengenezo ya Barabara shilingi bilioni sita nukta sita zilitumika kwa ajili ya kufungua barabara mpya, kufanya matengenezo ya kawaida na matengenezo ya sehemu korofi na kwamba miradi yote imekamilika.