Back to top

Bilioni 3 na Milioni 700 zatolewa kwa ajili ya ujenzi wa maji Busega.

18 September 2020
Share

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhe.Kassim Majaliwa amesema Shilingi bilioni 3 na Milioni  700 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji katika Wilaya ya Busega.

Ametoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata za Mkula na Lamadi, Wilaya ya Busega, Mkoani Simiyu wakati akiwa njiani kwenda Wilayani Bunda, Mkoani Mara.

Mhe.Majaliwa amesema fedha hizo zimetumika kujenga mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Lukungu ambao tayari umekamilika.

Ameitaja miradi mingine kuwa ni mradi wa maji bomba Kiloleli unaohudumia vijiji vitatu vya Ihale, Ijitu na Yitwimila B ambao pia umekamilika.

Kuhusu umeme, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kati ya vijiji 59, vijiji 53 vimeshapelekewa huduma ya umeme, na vijiji sita bado havina umeme.