Back to top

Bima za kughushi zatafuna magari ya abiria mkoani Ruvuma

12 April 2019
Share

Ukaguzi wa magari mkoani Ruvuma uliofanywa na mamlaka ya usimamizi wa bima  nyanda za juu kusini kwa kushirikiana na jeshi la polisi umebaini baadhi ya magari kutumia stika za polisi  za kughushi huku magari mengine ya abiria yakitumia bima za magari ya kutembelea nyumbani.

Ukaguzi huo umefanyika katika kituo cha mabasi cha Songea mkoani Ruvuma na kubaini kasoro hizo  hatua ambayo haikubaliki  kisheria na pia inaleta usumbufu kwa abiria pindi inapotokea ajali.

Kamanda  wa kikosi cha usalama bara barani  mkoa wa Ruvuma  mrakibu msaidizi wa polisi Salumu Morimori amesema suala la magari kuwa na bima ni takwa la kisheria na wanaokiuka takwa hilo pamoja na kuwa na stika za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wao madereva na abiria wamesema kuwa  zoezi la ukaguzi wa bima na stika za polisi kwenye magari ni muhimu sana kwa kuwa linawasaidia abiria kulipwa fidia zao pindi  itokeapo ajali  na madereva inawasaidia kutii matakwa ya kisheria.