Back to top

Binti atolea mimba gesti , adai aliyempatia aliikataa.

20 March 2020
Share

Binti mmoja mwenye umri wa miaka 18, Rehema Fabian, mkazi wa Mlali mkoani Morogoro ametoa mimba ya kichanga cha kiume kwenywe nyumba moja ya kulala wageni katika chumba alichokodi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafungwa, amekiri kupokea taarifa ya tukio hilo na kwamba binti huyo aliyedai amefanya hivyo baada ya mimba hiyo kukataliwa na kijana aliyempatia, ambaye ni mfanyakazi mwenzie katika mgahawa , amekutwa na madawa mbalimbali ya binadamu yakiwemo aliyokuwa akiyatumia kutoa mimba.

Kamanda Mutafungwa akatumia fursa hiyo kuwaonya wamiliki wa maduka ya dawa kuacha kuuza kiholela dawa badala yake wazingatie masharti ya leseni zao, sambamba na kuwashauri vijana kuacha kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi kabla ya kujipanga kwa maisha ya baadaye.