Back to top

Bodi ya nyama yabaini na kusitisha machinjio bubu Kibamba.

15 September 2019
Share

Bodi ya nyama nchini imebaini na kusitisha mara moja shuguli zote za uchinjaji pamoja uuzaji wa mifugo mbalimbali katika machinjio bubu yaliyopo eneo la Kibamba halmashauri ya wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam.

Hatua hiyo imekuja baada ya Kaimu Msajili wa bodi ya nyama kufanya ziara ya kushutukiza na kubaini maeneo hayo kuwa hayajakidhi viwango vya kisheria pamoja na kukosa vibali kutoka bodi hiyo na taasisi zingine za umma pamoja na mazingira yanayozunguka maeneo hayo kuwa machafu hali inayoweza kuleta magonjwa ya mlipuko kwa afya za binadamu.

Kwa upande wao baadhi ya wafanya biashara wa nyama katika machinjio hiyo bubu wameomba serikali kupitia halmashauri ya Ubungo kutenga maeneo na kuboresha mazingira hayo mapema ili waweze kuendeleza kuchangia katika kipato na kuinua uchumi nchi.