Back to top

Bunge lataka waliohujumu mabilioni katika taasisi za umma wawajibishwe

26 May 2020
Share

Bunge limeitaka serikali izichukulie hatua taasisi zote za umma ikiwemo Wizara ya Malisili na Utalii kwa matumizi mabaya ya mabilioni ya fedha kinyume na utaratibu.

Wakichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya (PAC ) iliyowasilishwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo hiyo baadhi ya wabunge wamesema fedha zilizotengwa kwa ajili ya Mradi wa Umeme  Vijijini( REA) zaidi ya bilioni  1.8 zimetumika vibaya.

Aidha wabunge hao wamesema kitendo cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kutumia zaidi ya bilioni 10 kununua vifaa vingi ambavyo havihitajiki  ni harufu ya rushwa.

Wabunge hao pia wamesema kuna haja  ya baadhi ya taasisi za serikali zinazodaiwa gharama za umeme na Tanesco walipe ili liweze  kujiendesha kiufanisi.