Back to top

Bweni lawaka moto Mwanza ,wanafunzi wanusurika.

23 July 2020
Share

Wanafunzi 36 wa shule ya wasichana ya Mtakatifu Joseph iliyopo jijini Mwanza wamenusurika kifo baada ya bweni moja la shule hiyo kuungua moto na kusababisha hasara ya mali na vitu mbalimbali vya wanafunzi.

Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Florida Busasi amesema tukio hilo la moto limetokea majira ya saa 11 alfajiri ya Julai 23 kwenye  bweni lenye vyumba vitatu vyenye uwezo wa kuchukua vitanda 18 ambapo wanafunzi hao wamepoteza kila kitu zaidi ya kubaki na nguo walizokuwa wamevaa .

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ambwene Mwakibete amesema uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo bado unaendelea.