Back to top

CHADEMA waitaka NEC kutenda haki uchaguzi mdogo wa ubunge Buyungu

12 July 2018
Share

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimeitaka tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) kusimamia kwa haki uchaguzi mdogo wa marudio wa ubunge wa jimbo la Buyungu na wamadiwani wa kata mbalimbali huku pia wakilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kuwakamata baadhi watu waliyoghushi sahihi za viongozi wa CHADEMA kwa lengo la kuhalalisha wagombea ambao chama hiko hakijawateuwa kugombea katika halmashauri ya Tunduma mkoani Songwe.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt.Vicent Mashinji amesema katika uchanguzi huo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Agosti 21 mwaka huu kumeanza kujitokeza kasoro mbalimbali huku akisema wagombea wa halmashauri ya Tunduma mkoa wa Songwa wamepitishwa kwa barua ya kughushi hivyo kuitaka tume na vyombo vya dola kuwachukulia hatua wote waliohusika na suala hilo.