Back to top

CHADEMA yamsimamisha Lissu kuwania Urais kupitia chama hicho.

04 August 2020
Share

Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umempitisha mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Tundu Lissu kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya chama hicho na Katibu Mkuu akitangaza rasmi kuwa fomu ya kugombea urais itachukuliwa tarehe Nane mwezi huu saa tano asubuhi makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dodoma.

Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA , Mhe.Freeman Mbowe amesema mwaka huu wamejipanga kushinda uchagauzi na hivyo akataoa tahadhari kwa mamlaka husika kuchukua hadhari za kina ikiwemo Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.

Naye Mhe.John Mnyika amesema tayari wameiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwapa taarifa za mgombea wao kwenda kuchukua fomu  pamoja na kuwataka wagombea wa nafasi zote za ubunge na udiwani kuchukua fomu siku ya kwanza kabisa ya uchukuaji pamoja na kuhakikisha wanasimamia ilani ya chama.

Katika mkutano huo waliohudhuria watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wawakilishi wa taasisi mbalimbali za umma na binafsi ambapo Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha ACT Wazalendo,  Maalim SEIF SHARIF HAMAD  amesema lazima wajipange ili washinde.