Back to top

Chama cha wanasheria Tanganyika chatakiwa kuhudumia wananchi.

21 August 2018
Share

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bwana AMON MPANJU amekitaka Chama cha Wanasheria Tanganyika kuwahudumia wananachi kulingana na miiko na kanuni taaluma yake badala ya kujigeuza wanaharakati wa siasa.

Akizungumza na wakufunzi wa mafunzo ya wafunzo ya wasaidizi wa sheria nchini amesema taaluma ya sheria ipo kwa ajili ya kujenga nchi na siyo kujikita kwenye uwanaharakati na malumbano ya kisiasa na serikali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria KALEB GAMAYA amesema chama hicho kimesaidi kutatua matatizo ya wananchi na wakati mwingine bila hata kufika mahakamani.

Naye Mwenyekiti wa Mawakili mkoa wa Dodoma MARRY MUNISI amesema awali wasaidi wa kisheria hawakukubaliwa na mawakili lakini sasa wamekuwa ni msaada mkubwa kwenye usuluhishi wa migogoro hasa maeneo ya vijijini .