Back to top

Chanzo cha kuadimika kwa mafuta ya Alizeti nchini chabainika.

11 January 2021
Share

Chama cha Wasindikaji Mafuta ya Alizeti nchini kimesema chanzo cha kuadimika kwa mafuta ya kupikia kumesababishwa na kunyesha kwa mvua nyingi katika mikoa 15 inayozalisha kwa wingi zao hilo.

Hali hiyo imesababisha  kuharibika kwa mbegu mashambani na kusababisha kushuka kwa mavuno katika msimu wa kilimo uliopita.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji Mafuta ya Alizeti nchini, Bwana Ringo Ringo ametoa tamko hilo Jijini Dodoma ikiwa ni siku chache tangua kuanza kuadimika kwa bidhaa hiyo katika maeneo mbalimbali.

Bwana Ringo amesema bado wanaendelea kufanya mazungumzo na serikali ili kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana kwa wingi na gharama nafuu.