Back to top

China kudhibiti mlipuko wa homa inayotokana na virusi vya CORONA.

31 January 2020
Share


China imesema ina imani kwamba itaweza kuudhibiti mlipuko wa homa inayotokana na virusi vya Corona huku idadi ya visa vilivyothibitishwa ikikaribia watu 10,000 duniani kote.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Hua Chunying amewaambia waandishi habari kwamba China itafanikiwa kupambana na changamoto zinazotokana na virusi hivyo vilivyoanzia nchini humo mnamo mwezi Disemba. 

Ameongeza kwamba China inashirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo limeutangaza mlipuko huo kuwa dharura ya afya ya Kimataifa. 

Hadi jana usiku, China imethibitisha vifo 213 vinavyotokana na homa ya virusi hivyo vya Corona, kulingana na WHO hamna mtu aliyefariki katika nchi nyingine licha ya kurekodiwa visa 98 duniani kote.