Back to top

China yaionya Uingereza kwa madai kuwa Corona imetengenezwa Huwan

06 May 2020
Share

Balozi wa China nchini Uingereza ameonya kuwa madai ya baadhi ya viongozi wa Uingereza kuwa virusi vya Corona vilitengenezwa katika maabara moja ya mji wa Wuhan nchini China, yataathiri uhusiano  wa nchi hizo mbili.

BaloziLiu Xiaoming amesema matamshi hayo kiholela ya baadhi ya wanasiasa wa Uingereza kuhusu chanzo cha virusi vya Corona kuwa ni maabara ya mji wa Wuhan yanatia sumu kwenye uhusiano wa nchi hizo.

Amesema kuingiza siasa kwenye suala la virusi vya Corona, kunaondoa hali ya kuaminiana na ushirikiano wa China na Uingereza.

Baadhi ya wabunge wa Uingereza wamechukua msimamo sawa na wa serikali ya Rais DONALD TRUMP wa Marekani kwa kuituhumu China kuwa inahusika katika kuenea  virusi vya Corona.

Aidha Shirika la Afya Duniani  limeyataja madai hayo ya Marekani kuhusu chanzo cha virusi vya corona kuwa ni dhana tu na kuongeza kuwa, hakuna nyaraka wala ushahidi wa kielimu unaothibitisha kuwa virusi hivyo  vimetengenezwa na China.