Back to top

Chombo cha uchunguzi wa anga cha Hayabusa2 chatua sayari Ryugu.

11 July 2019
Share

Chombo cha uchunguzi wa anga za juu cha Japani cha Hayabusa2 kimetua leo kwenye sayari ndogo ya Ryugu kwa ajili ya misheni isiyokuwa ya kawaida ya kukusanya sampuli za mwamba chini ya ardhi.
 
Shirika la Utafiti wa Anga za Juu la Japani JAXA limesema data kutoka kwenye chombo hicho cha uchunguzi zinaonesha kilitua kwenye sayari ndogo majira ya saa 4:20 asubuhi leo Alhamisi kwa saa za Japani.