Back to top

Corona yaua wawili Afrika Kusini, amri ya kubaki majumbani yaanze.

27 March 2020
Share

Jumla ya watu wawili wamepoteza maisha mapema asubuhi ya leo Machi 27,2020 wakati nchi hiyo ikiwa imeanza rasmi kutekeleza amri ya watu wote nchini humo kukaa majumbani mwao kuzuia maambukizi ya Corona.

Waziri wa Afya wan chi hiyo amesema wameamka na huzuni kubwa sana kufuatia taarifa ya vifo hivyo.

Amri ya watu kubakia majumbani mwao kwa wiki tatu ikiwa ni moja ya mikakati ya kutokomza ugonjwa huo wa Corona itakuwa chini ya uangalizi wa jeshi na yeyote atakaekiuka atafungwa kwa miezi sita au kulipa faini kubwa.