Back to top

CRDB kutumia vitambulisho vya wamachinga kama dhamana ya mkopo.

15 July 2019
Share

Uongozi wa benki ya CRDB umesema utaanza kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga wenye vitambulisho vilivyotolewa na Rais wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Joseph Magufuli ili kuwafanya wafanyabiashara hao wakuze mitaji yao.

Mkurugenzi Mtendaji mkuu wa benki ya CRDB nchini,Abdulmajid Mussa Nsekela amesema hayo mjini Morogoro baada kukutana na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja na wasio wateja, mawakala na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Morogoro.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Stephen Kebwe akawataka wafanyabiashara kutumia taasisi za kifedha kupata mikopo na kuchangamkia uwekezaji kwani Morogoro ina fursa  za kilimo na biashara.