Back to top

DC atishia kufunga shule kwa kukithiri ushirikina,wazazi wapiga kura.

18 July 2020
Share

Mkuu wa wilaya ya Musoma Vicent Naano ametoa wiki moja kwa wananchi wa kijiji  Kakisheri kata ya Nyakatende wilaya ya Musoma vijijini wanaojihusisha na matukio ya kishirikina kuacha vitendo hivyo haraka  na endapo vitandelea basi atafunga shule na kuwahamisha walimu wa shule ya msingi  Kambarage.

Shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na matukio yasiyo ya kawaida ikiwemo walimu kuingiliwa kimwili nyakati za usiku ,kulazwa nje na wanafunzi kudondoka ovyo na kupiga kelele.

DC Naano ametoa maagizo hayo baada ya  kutokea kwa tukio la wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo kuanguka  na kupiga kelele ,kukuta  chakula aina ya makande kikiwa kimewekwa chooni  hali iliyowalazimu walimu ,wazazi na wanafunzi kupiga kura ili kubaini anayefanya matukio hayo kwa imani ya kishirikina.