Back to top

DC Naano atoa siku 3 kwa wavuvi haramu kujisalimisha kabla ya msako.

26 November 2020
Share

Mkuu wa wilaya ya Musoma Dk.Vicent Naano ametoa siku tatu kwa wavuvi haramu wote kujisalimisha kabla ya msako wa nyumba kwa nyumba haujaanza huku akidai uvuvi haramu umerudi kwa kasi kiasi ambacho kinapelekea serikali kupoteza zaidi ya shilingi bilioni moja kwa mwezi kwa samaki aina ya Sangara pekee na kusababisha viwanda vya samaki kufa kwa kukosa samaki.

Akizungumza na ITV siku moja baada ya kufanya kikao na watendaji vijiji kata na watendaji wa idara ya uvuvi Dk.Naano amesema zoezi hilo litaanza leo na kuwataka wale wote waliona nyavu hizo kuzisalimisha kabla hawajakamatwa na mkono wa sheria.

Awali akizungumza na wenyeviti, watendaji wa vijiji, kata na watendaji wa idara ya uvuvi Dk.Naano amesema kukithiri kwa uvuvi haramu ndani ya ziwa Victiori kunaathiri mapato ya serikali.