Back to top

DENIS ONYANGO ATANGAZA KUSTAAFU TIMU YA TAIFA.

13 April 2021
Share


Golikipa wa timu ya taifa ya Uganda Denis Onyango ambaye anakipiga katika klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Uganda.

Denis Onyango alianza kuitumikia timu ya Uganda tangu mwaka 2005 wakati akiwa katika klabu ya Villa SC ya Uganda na hadi sasa akiwa katika klabu ya Mamelod ametangaza kustaafu baada ya kuidakia timu yake ya taifa ya Uganda katika jumla ya michezo 75.

Na sasa Onyango atakuwa akiitumikia klabu yake ya Mamelod iliyotinga robo fainali ligi ya mabingwa Afrika huku akiwa hana jukumu la timu ya taifa baada ya kutangaza kustaafu.

Mastaa kibao wa timu ya taifa ya Uganda kama Emanuel Okwi, Josef Owino na Hamis Kiiza wamecoment na kumtakia kila la kher golikipa huyo.