Back to top

Denmark yasitisha utoaji Chanjo ya Covid-19 ya Oxford ya AstraZeneca.

15 April 2021
Share

Denmark imesitisha utoaji wa chanjo ya Covid-19 ya Oxford ya AstraZeneca kutokana na ripoti za athari ya kuganda kwa damu, ikiwa nchi ya kwanza ya Ulaya kuchukua hatua hiyo.

Hatua hii itafanya programu ya kutoa chanjo ichelewe kwa majuma kadhaa.

Shirika la Uangalizi wa dawa barani Ulaya juma lililopita lilitangaza uwepo wa uwezekano wa athari za kuganda damu ukihusishwa na chanjo, lakini walisema hatari ya kufa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 ni mkubwa, pamoja na kuwepo kwa athari hizo.