Back to top

Dereva,utingo wateketea kwa moto Morogoro.

22 July 2020
Share

Watu wawili dereva na utingo wake wamefariki dunia kwa kuteketea kwa moto baada ya roli lenye namba za usajili T.177 AJN lililosheheni mafuta ya petroli na dizeli kuacha njia, kupinduka kisha kuwaka moto na kuteketea katika eneo la Mkongeni Dakawa mkoani Morogoro wakati likitokea jijini Dar es alaam kuelekea wilayani Gairo.

Akitoa taarifa ya ajali hiyo Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro ACP Mugabo Wekwe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mara moja.