Back to top

Dhahabu yakamatwa yakisafirishwa kinyume na sheria Handeni.

22 March 2019
Share

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Handeni ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe imekamata zaidi ya gramu mia moja na themanini za madini aina ya dhahabu ambayo yalikuwa yanasafirishwa nje ya wilaya kinyume na utaratibu.

Akielezea tukio hilo Afisa madini wilaya ya Handeni Bw.Zefania Kalunde amesema kuwa walipata taarifa hiyo kutoka kwa wasamaria wema ndipo wakachukua jukumu la kwenda kukamata madini hayo kwenye kambi iliopo kwenye mgodi wa dhahabu wa Magambazi ambao upo nje kidogo ya mji wa Handeni.

Mkuu wa wilaya ya Handeni ambae pia ndiye Mwenyekiti wa kamati ya usalama ametoa onyo kwa wachimbaji wote wa madini wilayani humo kuhakikisha wanafuata kanuni na utaratibu wa sheria za madini hasa kwenye usafirishaji.