Back to top

Dkt Shein ateua mrithi wa Jecha ZEC

20 June 2018
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein amemteua Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Hamid Mahmud  kuwa Mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar-ZEC

Tarifa iliyotolewa Ikulu jioni hii na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Abdulhamid Yahya Mzee mbali ya kumetua Mwenyekiti mpya amabye pia kwa hivi sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa – NEC Dkt.Shein pia amewataeua Makamishna wa tume hiyo ambao ni Mabruki Jabu Makame aliyeawahi kuwa katibu mkuu Ofisi ya Waziri Kiongozi, Fateh Saad Mgeni, Jaji wa Mahakama kuu Khmis Ramadan Shabaan, Makame Juma Pandu, Dkt.Kombo Khamis Hassan na Bi.Jokha Khamis Makame,watendaji hao wataapishwa ijumaa Ikulu.

Tume hiyo inatarajiwa kazi yake ya kwanza na kusimamia uchaguzi mdogo wa jimbo la Jang’ombe ambalo liko wazi baada ya mwakilishi wake Abdulah Maulid Diwani kufukuzwa  ndani ya chama cha Mapinduzi baada ya kukiuka maadili ya chama.