Back to top

DPP awafutia mashtaka mfanyabiashara Yusufali na wenzake 4.

11 January 2019
Share

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameifuta kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa ikimkabiri mfanyabiashara Yusufali na wenzake 4 ambao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka 198.

Akizungumza mbele ya hakimu Agustina Mbando,wakili wa serikali Hashimu Ndole ameieleza Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.

Amesema kwa taarifa hiyo inaletwa mahakamani hapo chini ya kufungu cha 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 na marejeo yake ya mwaka 2002.

Hakimu mkazi Agustina Mbondo ameifuta keshi hiyo, na washtakiwa wamekamatwa tena na watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka mapya.