Naibu Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) amekanusha taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya Kijamii zikidai kuwa Msuluhishi wa mgogoro wa Burundi Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa amelalamika kukosa ushirikiano wakati alipokuwa anafanya kazi ya usuluhishi wa mgogoro huo
Akizungumzia taarifa hizo za mitandao ya kijamii Jijini Arusha Naibu katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Mhandishi Steven Mlote amesema ni za uzushi na zinapaswa kupuuzwa kwani zinatolewa na watu wasioitakia mema Jumuiya hiyo
Aidha Mhandisi Mlote amefafanua kuwa Mhe.Mkapa alishamaliza kazi yake na kuikabidhi kwa wakuu wa nchi wanachama ambao licha ya kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya na pia walipongeza ushirikiano mkubwa uliotolewa na sekretarieti ya Jumuiya hiyo wakati wote wa mazungumzo
Bw.Mlote amesema kimsingi Jumuiya ya Afrika mashariki haina tatizo lolote na aliyekuwa msuluhishi wa Mgogoro huo na kwamba kwa sasa inaendelea kutekeleza maelekezo ya wakuu wan chi wanachama yakiwemo ya kuongeza kasi ya kusimamia miradi mbalimbali ya kuwaunganisha wananchi wa nchi wanachama kiuchumi kijamii na kisiasa
Taarifa zinazoenea kwenya baadhi ya mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa aliyekuwa msuluhishi wa Mgogoro wa Burundi amelalamika kuwa alikosa ushirikiano wa watendaji wa Jumuiya hiyo wakati wa mazungumzo hayo .