Back to top

"Elimu bure kufika chuo kikuu"

14 June 2018
Share

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema mpango wa elimu bure utazidi kuwanufaisha wanafunzi wengi zaidi nchini kadri Serikali inavyopata fedha ambapo kwa sasa mpango huo wa elimu bure unaishia kidato cha nne lakini huenda ukafika mpaka vyuo vikuu kama fedha zitapatikana.

Amesema kwa sasa Serikali inazidi kujiimarisha katika ukusanyaji wa mapato ili kuwezesha fedha zaidi kupatikana na kufanikisha masuala mbalimbali ikiwemo la elimu bure.

Naibu Waziri Ole Nasha alikuwa akijibu swali ambalo lilielekezwa kwa wizara yake kuhusiana na mpango wa elimu bure na mkakati wa Serikali kuhakikisha wanafunzi wote wa ngazi zote wanapata elimu bure.