Back to top

"Ethiopia inaongoza kukamatwa raia wake kama wahamiaji haramu".

24 May 2018
Share


Idara ya Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam imeitaja nchi ya Ethiopia kama taifa linaloongoza kwa kukamatwa raia wake kama wahamiaji haramu na kubainisha kuwa tayari kuna mazungumzo na viongozi wa taifa hilo juu na namna ya kudhibiti tatizo hilo.

Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam Crispin Ngonyani amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amebainisha kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Mei mwaka 2018 jumla ya wahamiaji haramu 602 walikamatwa  227 kati yao ni Waethiopia. 

Ameongeza kuwa idadi kubwa ya wanaokamatwa nchini wanataja kuwa wanapita kwenda Afrika ya Kusini huku akitoa onyo kwa Watanzania wanaoshiriki kuwasaidia.