Back to top

EWURA yawahakikishia usalama watumiaji wa Petroli na Dizel

22 June 2018
Share

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji nchini - EWURA - imewahakakishia Watanznia na watumiaji wa mafuta ya Petroli na Dizel kuwa nishati hiyo itaendelea kuwa salama kama ilivyo sasa.

Mamlaka hiyo imewataka wananchi kutoa taarifa kwa yeyote anayejaribu kufanya uchakachuaji na kero nyingine zinazotokana na matumizi ya mafuta, maji pamoja na umeme.

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi Mkuu wa Mafuta, Kanda ya Mashariki, Bwana NATHANAELI EDWARD wakati wa mafunzo kuhusu majukumu na kazi za EWURA kwa watendaji wa Kata na mitaa wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro .

Kwa upande wao baadhi ya Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa waliohudhuria mafunzo hayo wamesema wamekuwa wakikabiliwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya kero za maji na umeme na kushindwa kuzitatua kutokana na kutokuwa na elimu juu ya masuala yanayohusu nishati.