Back to top

Familia yagoma kuzika mwili kwa siku 30 Kilombero.

27 May 2020
Share

Familia ya mzee Mapondera iliyopo kijiji cha Mrabani halmashauri ya mji wa Ifakara wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, imeendelea kusota na mwili wa kijana wao Kelvin Mapondera mwenye umri wa miaka 22 bila kuzikwa yapata siku ya 30 sasa tangu alipofariki.

Wakizungumza kwa masikitiko wazazi wa marehemu Kelvin Mapondera wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli kuingilia kati sakata hilo ili waweze kumzika mpendwa wao.

Wanafamilia hao wameeleza kusikitishwa na hatua ya kunyimwa taarifa ya kifo cha kijana wao kwani wamejaribu kufuata taratibu zote za kudai taarifa hiyo lakini jitihada hizo hazijazaa matunda.

Kufuatia hali hiyo Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema hatua mbalimbali zimeanza kuchukuluwa na amewatakaa ndugu wa marehemu kuzika mwili huo.