Back to top

Fundi Selemala mlemavu wa macho ashangaza wengi Songea

19 April 2019
Share

Fundi Selemala mlemavu wa macho mkazi wa Msamala mjini Songea mkoani Ruvuma Bw.Yusuph Linyama amewaduwaza watu wengi kwa kumudu  kazi hiyo licha ya ulemavu wa macho alionao ambapo ameomba  kusaidiwa  mtaji ili aweze  kufungua darasa na kusaidia walemavu wenzake.

Bw.Yusuph Linyama ambaye  aliupata ulemavu huo baada ya kuhitimu darasa la saba ambapo licha ya ulemavu wake wa macho anajishughulisha na shughuli hiyo ya ufundi anatoa wito kwa wazazi kuwasomesha watoto wao wenye uleamavu kama ambavyo wazazi wake walivyomsomesha yeye ufundi selemala.