Back to top

Gari ya mgombea mwenza CHADEMA yapata ajali Kahama.

21 September 2020
Share

Gari alilokuwa anatumia Mgombea Mwenza nafasi ya Urais kupitia CHADEMA Salum Mwalimu limepata ajali katika eneo la Msoka Kata ya Ngogwa wakati wakitoka kwenye mkutano wa Kampeni jimbo la Msalala kuelekea kwenye mkutano wa Kahama.

kwa mujibu Afisa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA Tumaini Makene ni kwamba wote waliokuwa kwenye gari hiyo wako salama na Mgombea mwenza wa Urais wa chama hicho anaendelea na kampeni Kahama.