Back to top

Gari yakwamisha safari kwa saa sita katika mto Nkana mkoani Songwe.

13 September 2018
Share

Madereva wa gari za mizigo wamejikuta katika wakati mgumu usiku wa manane baada ya gari moja kukwama kwa zaidi ya masaa 6 katika mto Nkana unaotenganisha vijiji vya Ntinga na Chindi katika kata ya Msangano wilaya Momba mkoani Songwe.

Changamoto iliyosababishwa na kukosekana kwa daraja kubwa la kuunganisha mawasiliano ya barabara ya Chiwezi inayotoka mjini Tunduma hadi Chitete yaliyoko Makao Makuu ya wilaya ya Momba.