Back to top

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na Zambia wakutana Tunduma

21 September 2018
Share

Magavana wa Benki kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga na Benki  kuu ya Zambia Dk. Danny Kalyalya wanatarajia kukutana leo mpakani Tunduma mkoani Songwe, na kutia saini makubaliano ya kuruhusu matumizi ya  Shilingi ya Tanzania na Kwacha ya Zambia, lengo ni kukomesha biashara holela ya fedha za kigeni mpakani hususani kwenye forodha za Tunduma na Nakonde.

Hatua hii inalenga pia kuchochea ushindani wa haki kwa taasisi za fedha hasa mabenk na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni na kuziwezesha benki  kuu kuimarisha ujazi wa fedha katika soko.