Back to top

Genge la matapeli wakamatwa mjini Bujumbura nchini Burundi  

14 January 2019
Share

Jeshi la polisi nchini Burundi limewakamata watu waliokuwa wakiwatapeli  raia kwa kutumia majina ya viongozi wa ngazi za juu nchini humo kama rais,spika wa bunge,  baraza la seneti, na viongozi wengine.

Mkuu wa kitengo cha kupambana na uhalifu kwenye jeshi la polisi nchini humo  Manisha Emile amesema kuwa genge hilo la matapeli linaundwa na makundi mawili ambayo moja hutumia ujanja wa kuuza dhahabu na kundi nyingine kuwatapeli raia kwa kutumia uhalifu mtandaoni kwa kujipa vyeo vya wakuu nchini humo kukiwemo Mh Rais,mkwe,spika wa bunge ima ule wa baraza la seneti na wengine.

Hali hiyo ya wizi kwa kutumia ujanja umekithiri nchini humo hususani jijini  Bujumbura ambapo mara kwa mara watu hupata ujumbe kupitia mitandao ya kijamii wakifahamishwa kuwa wamepata ajira na kutakiwa kutuma pesa na mara kadhaa wanaotumia ujanja huyo wanakuwa wapo jela.